(Swahili) Ripoti hii iliandaliwa na umoja wa shirika za kiraia za DRC na Ulaya. Ni muendelezo wa ripoti ya mwezi wa Juni mwaka 2015 ambayo ilitoa tahadhari kwa jumuiya ya kimataifa juu ya ukiukwaji wa haki za binadamu, umaskini,unyonyaji wa ajira na kupokonya ardhi unafanyika ndani ya maeneo ya mkataba inadaiwa na kampuni, kama vile viungo iimarishwe na mwisho na muhimu utu wa kisiasa wa DRC. Pamoja na maswali yaliyotolewa na ripoti hii,DFIs ambaye awali imewekeza katika FERONIA iliendelea na mfuko wa biashara. Mnamo Desemba 2015, DFIs zingine kadhaa zimekubaliana kushiriki katika duru mpya ya kutoa jumla ya $ milioni 49. Katika hii ripoti, tunaletaushahidi nyingine za uuzaji wa mashamba kimagendo, na mbinu duni za kazi za FERONIA. Tunafunua kwa mara ya kwanza jinsi kampuni ilitumikisha mfumo wa kipesa uliokuwa utata na usio wazi kwa kuendesha kimagendo fedha kutoka DFIs. Ripoti hii inaonyesha makosa yenyi kutisha kuhusu matumizi ya fedha za uma na IFD ambayo yote hudai kuwajibika kwa kuzingatiya viwango vikali vya uwekezaji. Tunaomba pia uchunguzi huru wa kimataifa kwa kutafuta ukweli zidi ya ukiukaji wa haki za binadamu, na ukiukwaji mwingine unaodaiwa kufanywa na kampuni dhidi ya jamii. Kwa kuonekana kushugulika vilivyo, DFIS, kama vile nahisa mkuu wa kampuni FERONIA na mfadhili mkuu wa fedha wa kampuni, inapashwa kuchukuwa hatua za haraka na kutangaza akaunti zote za FERONIA na zile za kila mmoja wa matawi zake pamoja na nyaraka za kisheria ambazo FERONIA anajidai kupewa kwa kumiliki sehemu ile ya udongo katika DRC.
Pia waandishi wa ripoti hii wanaomba kwa FERONIA pamoja na mashirika yenye kuhifadhi maendeleo wayasikilize malalamiko za wakaaji husika ambao kwa muda mrefu wanadai kurudishiwa mara moja sehemu za udongo
wao na kulipwa fidiya.